DEAL DONE: Chelsea yakamilisha Usajili wa Mlinda Mlango wa Fulham.

 


Chelsea imethibitisha kumsajili kipa, Marcus Bettinelli kwa uhamisho huru kufuatia kumaliza mkataba wake na Fulham.


Bettinelli 29" kasaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia The Blues...Atatoa ushindani kwa Edouard Mendy na Kepa Arrizabalaga huko Stamford Bridge na kuchukua nafasi ya Willy Caballero, ambaye ametemwa msimu huu wa joto.


Bettinelli alitumia msimu wa 2020/21 kwa mkopo huko Middlesbrough, akicheza mechi 42 walipomaliza nafasi ya 10 kwenye Championship.... Ndio usajili wa kwanza wa Chelsea tangu walipokuwa mabingwa wa Ulaya kwa mara ya pili mnamo Mei.

Post a Comment

0 Comments