Dondoo Mbalimbali Za Soka Afrika leo July 29.2021

 


✍️šŠš„š’šˆ š˜š€ šŒšŽš‘š‘šˆš’šŽš šŠš”š’šˆšŠšˆš‹šˆš™š–š€ Lš„šŽ 

Mahakama ya usuluhisho wa michezo (CAS) kupitia tovuti yake imechapisha taarifa ya kesi zitakazosikilizwa leo July 29 katika mahakama hiyo na miongoni mwa kesi hizo ni ile ya Yanga Sc dhidi ya mchezaji wa Simba Sc, Bernard Morrison

✅Klabu ya Horoya AC ya Guinea imethibitisha kukamilisha umsajili mshambuliaji kinda raia wa Senegal Pape Abdou Ndiaye mwenye umri wa miaka 19 kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka klabu ya ASC Jaraaf ya Senegal.

✍️MANARA 'OUT' NAFASI YA USEMAJI SIMBA SC 

Wakati huohuo Bodi Ya Wakurugenzi ya klabu ya Simba Sc imeridhia matakwa ya Haji Manara ya kutoendelea kuhudumu katika nafasi ya Msemaji wa Klabu. 

Klabu ya Simba Sc imemteua Ndugu, Ezekiel Kamwaga kuwa Kaimu Mkuu Wa Idara Ya Habari Na Mawasiliano kwa kipindi cha miezi miwili.


✍️Habari kutoka Misri zinaeleza kuwa Al Ahly washatuma ofa ya USD milioni 2 (Tsh Bilioni 4) kwa ajili ya kuishawishi Simba SC imuachie Luis Miquissone (26) ajiunge nayo


✍️Taarifa iliyorasmi klabu ya Yanga Sc imeachana na beki wake wa kati Lamine Moro raia wa Ghana.


✅Kocha wa zamani wa @FcLipuli Nzeyimana Mailo Ismail raia wa Burundi amejiunga na klabu ya Vital'O. Mailo, ambaye inasemekana alikuwa kwenye rada ya @EtincellesFC, atakuwa Vitalo FC kwa msimu wa 2021-2022.


✍️Kampuni ya Be Sports Management inayomsimamia mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo na klabu ya Al Masry ya Misri Francy Kazadi Kasengu imesema kuwa mshambuliaji huyo ni mchezaji halali wa klabu ya Al Masry sio Wydad Casablanca ya Morocco.

Kampuni hiyo imedai kuwa hakuna mazungumzo yoyote na klabu ya Yanga SC ya Tanzania kuhusu usajili wa nyota huyo ambaye ana mkataba na Al Masry mpaka June 2024. Pia ameongeza kuwa thamani ya Kazadi kwa sasa ni dola 300,000 (milioni 695.7 za Kitanzania)

✍️Beki wa kushoto Luzolo Sita raia wa DR Congo tayari yupo mjini Lubumbashi kukamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya TP Mazembe kwa mkataba wa miaka mitatu kama mchezaji huru baada ya mkataba wake na klabu ya As Vita kuisha.

✍️Timu anayochezea nyota wa kitanzania Shaaban Idd Chilunda ya Moghreb Tetouan jana rasmi imeshuka daraja baada ya kukubali kichapo ya mabao 3-2 dhidi ya RS Berkane

✍️Klabu ya Maritzburg United FC ya Afrika Kusini imekamilisha usajili wa mshambuliaji raia wa Ghana Richard Agbalegah Zumah kutoka klabu ya San Pedro Fac ya Ivory Coast.

✍️Onyango atajwa kwenye kinyang’anyiro cha Beki Bora #CAFCL msimu huu

Post a Comment

0 Comments