Haruna Niyonzima amtabiria makubwa Waziri Junior

 

Kiungo Haruna Niyonzima amesema anavutiwa na mshambuliaji Waziri Junior akiamini wakati wake wa kung'ara utafika

Waziri alifunga mabao mawili katika msimu uliopita akiwa ametumika katika michezo michache

Niyonzima amesema Waziri ni mchezaji mwenye jitihada, uwezo wake haujaonekana kwa sababu hakuwa akipata nafasi ya kucheza mara kwa mara

"Nampenda bwana mdogo Waziri Junior ni mchezaji mwenye jitihada lakini hajapata nafasi ya kuonesha uwezo wake. Hata tukiwa mazoezini kuna vitu anavifanya naona ni mshambuliaji mzuri," >>>.alisema Niyonzima

Yanga Sc ilimsajili Waziri kutoka klabu ya Mbao Fc ambayo aliifungia mabao 17 katika mashindano yote msimu wa 2019/20

Bado ana mkataba wa mwaka mmoja na mabingwa hao wa kihistoria

Post a Comment

0 Comments