Uongozi wa klabu ya Azam FC umetangaza kufikia makubaliano ya pande mbili ya kuachana na wachezaji wao wanne wa kimataifa.
Wachezaji hao ni beki wa kati, Yakubu Mohammed, kiungo Ally Niyonzima, mshambuliaji Mpiana Monzinzi na Obrey Chirwa, ambaye mkataba wake umemalizika.
Azam FC inawashukuru wachezaji hao kwa mchango wao waliotoa katika klabu hii bora kipindi chote walichokuwa nasi na tunawatakia kila la kheri huko waendako.
0 Comments