TAFAKARI MUHIMU MUDA HUU WA USAJILI

 


✍️Hebu tuwe serious kidogo katika hili, club ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika ya Kusini ni mara yao ya kwanza kufuzu fainali ya CAF Champions League, tunatambua hii Kaizer Chief iliyofika hatua hiyo na kukipiga dhidi ya Al Ahly ya Misri, hawakua imara saana wala kuwa na kiwango kile cha zaidi ya Mamelod Sundowns na timu zingine za S.A


✍️Kitu kingine cha kujifunza ni Kaizer bado hawajaridhika na kile kilichotokea pale Morocco na sasa wametoa majina ya wachezaji 7 wanaoachana nao ambao ni


1⃣Lazarus Kambole

2⃣Stalwart Willard Katsande

3⃣Brylon Peterson (Kipa)

4⃣Siposakhe Ntiya-ntiya

5⃣Yagan Sasman 

6⃣Kgotso Moleko

7⃣Philan Zulu


Huku wakiongeza mikataba ya wachezaji wao mashuhuri kama Parker, Manyama na wengine.


✍️Ninavyo-ona watakuja na mikakati mipya kuanzia kwenye usajili wa maana kuelekea kwenye msimu wa 2021-22 ili kujenga kikosi chenye ubora wa kupambania kombe la ligi dhidi ya Sundowns na wengine hapo S.A


✍️Ili kuwa bora uwanjani ni lazima ubora uanzie nje hasa kwenye kufanya sajili, kuwa bora kwenye uchumi wa timu na ili kufanikisha yote hayo umoja na mshikamano wa management, mashabiki, wachezaji na wadau wote ni muhimu.


✍️Kutoka kwa Kaizer Chief na vilabu vingine hili ni somo la bure kwetu kujifunza wapi pa-kuanzia


Swali ni tumejifunza nini? Haya ni maswali ya kujiuliza.


✍️Je tunahitaji kusajili wachezaji wa aina gan? 


✍️Je ni yapi malengo yetu, tunahitaj kufika wapi na tupate nini katika hayo malengo? Kikombe gani na hatua gani, wapi na lini?


✍️Je, usajili tunaotaka kuufanya na wachezaji watakaobaki watatufikisha kwenye malengo hayo hasa tukilinganisha na ushindani tutakaokutana nao ndani ya ligi na ule wa kwenye mashindano ya kimataifa? 


✍️Haya ni Maswali machache Ila ni ya msingi kujiuliza kabla ya kumsajili wala kumuacha mchezaji yeyote huku tukibaki kutafakari pia kuwa tutakaokutana nao katika mashindano wanajiimarisha zaidi ili wawe tishio zaidi ya sasa.


Powered by @msukuma_wa_dutwa

Post a Comment

0 Comments