Chilunda ndo basi tena Morocco

 


Klabu ya Moghreb Tetouan anayoichezea Mtanzania Shaaban Chilunda imeshuka daraja jana usiku baada ya kupokea kichapo cha 3-2 dhidi ya RS Berkane kwenye Ligi Kuu ya nchini Morocco.

Chilunda amejiunga na timu hiyo msimu huu lakini ameifungia mabao mawili tu na kushindwa kuisaidia kuhakikisha wanabaki kwenye Ligi Kuu ya Morocco.

Wakati Chilunda mambo yakienda kombo, upande wa Simon Msuva kwake ni freshi kwani Wydad tayari wametangazwa kuwa mabingwa.

Post a Comment

0 Comments