Baraza la Mitihani la Tanzania linapenda kuwajulisha watu wote wanaotaka kufanya Mtihani wa Kidato cha Sita (ACSEE) mwezi Mei, 2022 kama Watahiniwa wa Kujitegemea kwamba;
1. Kipindi cha usajili kwa watahiniwa wa Kujitegemea kimeanza tarehe 01 Julai hadi 30 Septemba, 2021 kwa ada ya Shilingi 50,000/=. Aidha watakaojisajili kwa kuchelewa yaani tarehe 01/10/2021 hadi tarehe 30/10/2021 watalipa Shilingi 65,000/= ikiwa ni ada ya kawaida pamoja na faini.
2. Kabla ya kujisajili kwenye mtandao, waombaji wanapaswa kwenda kwenye Vituo vya mitihani kuchukua namba rejea (Reference number) zinazotolewa bure na kufanya malipo ya ada kupitia Posta au Benki kwa kutumia ‘Control Number’.
3. Ufafanuzi kuhusu utaratibu wa hatua za kufuata katika kutengeneza ‘Control Number’ na kujisajili, umetolewa katika tovuti ya Baraza la Mitihani la Tanzania:www.necta.go.tz. Aidha, kwa watahiniwa ambao hawataweza kutumia mfumo huo wafike ofisi za Posta au wapige simu 0738785945 kwa msaada zaidi.
4. Waombaji wote wanasisitizwa kuhakikisha wanajisajili mapema kwani mfumo wa usajili utafungwa baada ya kipindi cha usajili kumalizika.
0 Comments