Yanga warudisha Fadhira kwa Mashabiki.

 



Uongozi wa Klabu ya Yanga, unatoa shukrani za dhati kwa Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wake kwa ushirikiano mkubwa walioutoa kwa Klabu katika kuisapoti timu yetu kwa hali na mali katika msimu 2020/2021 uliomalizika.


-Yanga imejengwa katika misingi ya Umoja na Mshikamano na kwa hakika msimu huu Wanayanga wameonyesha kuwa na umoja na mshikamano wa hali ya juu katika masuala mbalimbali yaliyohusu maslahi ya klabu ya Yanga, hivyo uongozi hauna budi kuwashukuru Wanayanga wote kwa hilo.


 -Aidha, uongozi wa Yanga unatoa shukrani za kipekee kwa wadhamini wetu; SportPesa, Taifa Gas, Maji ya Afya, Azam TV pamoja na wadhamini na wafadhili GSM ambao kwa pamoja walishiriki vema katika kufanikisha msimu huu na mafanikio yaliyopatikana ni kutokana na mchango mkubwa wa wadhamini wetu.


-Uongozi pia unatoa shukrani kwa wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma zikiwemo hoteli,

Mashirika ya ndege, Watoa huduma za mabasi, mabenki yote yanayofanya kazi na Yanga, pamoja na wadau wengine wote kwa ushirikiano mzuri walioipatia klabu yetu.


-Mwisho Uongozi wa Yanga unaomba Wanachama, Wapenzi na Mashabiki, Wadhamini na Wadau wengine wote kuendeleza Umoja, Mshikamano na Ushirikiano katika msimu mpya wa Ligi 2021/2022 ambapo pia Yanga itashiriki michuano ya Kimataifa.

Post a Comment

0 Comments